Jumanne 29 Aprili 2025 - 20:33
Wosia Maalumu wa Allama Tabatabai Kuhusiana na Mabinti (watoto wa kike)

Allama Tabatabaei (r.a), kwa heshima na mapenzi ya kipekee kwa mabinti zake, alikuwa akisisitiza juu ya utulivu, furaha, na malezi sahihi kwao, na alikuwa akiamini kuwa mwenendo huu humletea Mwenyezi Mungu pamoja na Mtume (s.a.w) furaha.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kutokana na mnasaba wa siku ya Binti chini Irani, tunasoma muhtasari wa simulizi ya heshima ya Allama Ṭabāṭabā’ī (r.a) kwa mabinti zake, huku akisisitiza mapenzi, utulivu, na malezi sahihi kwao:

Heshima Maalumu ya Allama Tabatabaei (r.a) kwa Mabinti wake

Katika mwenendo wa kimaisha wa Allama Tabatabaei (r.a) imeandikwa kuwa alikuwa akiwaheshimu mabinti wake kwa kiwango cha juu zaidi, na alikuwa akisema: “Mabinti wanapaswa kuonyeshwa mapenzi zaidi, ili wawe na furaha katika maisha ya baadaye, na waweze kuwa wake wema na wazazi wanaostahiki.”

Binti wa Allama Tabatabaei (r.a) anasimulia: “Wakati mwingine tulikuwa tukipika chakula ambacho kilikuwa kinaharibika kidogo; lakini baba yangu hakuwa hata akionyesha lolote, bali alikuwa akikisifia mno!”

Alikuwa akimwambia mama yangu: ‘Mabinti ni amana kutoka kwa Mungu, kila mtu atakayewaheshimu hawa, basi Mwenyezi Mungu na Mtume wanafurahu.’

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha